Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Kumbukumbu ya Raila Odinga imetoa onyo dhidi ya kutafuta fedha kwa kutumia jina la familia au kamati hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kiongozi huyo hayati mwezi huu. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Adams Oloo, alisema wamepokea taarifa kwamba watu wasio waaminifu wanatumia fursa ya maadhimisho hayo kuchangisha fedha kinyume cha sheria, na akawataka kukomesha tabia hiyo. Pia, kamati imewaalika Wakenya kutoka nyanja zote kushiriki katika shughuli hizo za maadhimisho.

ADAMS OLOO - WELCOME