Hakuna Mkenya, bila kujali anakoishi, atakayebaguliwa anapotafuta vitambulisho na kadi za kupigia kura, Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amesema. Aliwakemea wanasiasa wanaopinga utoaji wa kadi za kupigia kura kwa Wakenya walio nje ya mipaka ya nchi, akisema utawala wa Kenya Kwanza hautawahi kuathiriwa na ubaguzi kama huo. Alisema kitambulisho ni haki na lango la ajira, huduma za serikali na fursa katika kufanya maamuzi ya kitaifa.

KIPCHUMBA MURKOMEN - UGANDA