Viongozi wa Pwani wametangaza kuunga mkono azma ya Rais William Ruto ya kuchaguliwa tena, wakitaja rekodi yake ya maendeleo. Wakiongozwa na Waziri wa Madini Hassan Joho pamoja na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, viongozi hao wanasema watawahamasisha wakazi kumpigia kura Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Walizungumza hayo mjini Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta, wakati wa zoezi la kugawa hati miliki, huku Rais akiendelea na ziara yake ya maendeleo katika eneo la Pwani.
VOX POP – VIONGOZI