Timu ya Harambee Stars itafanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi ya leo jijini Conakry kabla ya mechi yao ya pili ya kufuzu kwa michuano ya AFCON ya mwaka 2027 dhidi ya wenyeji Guinea jioni hii. Stars, ambao tayari wamefuzu kwa michuano hiyo kama wenyeji, walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Eritrea, na kocha Benni McCarthy atakuwa akisaka ushindi wake wa kwanza katika Kundi D. McCarthy analenga kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kundi hilo huku wakijiandaa kwa michuano hiyo mwakani. Huyu hapa McCarthy.

BENII McCARTHY - STARS

Kocha Mkuu wa Mombasa United, Abdulhamid Moallin, ameahidi kuwapa upinzani mkali Kariobangi Sharks katika mechi ya mchujo ya Ligi Kuu ya FKF inayosubiriwa kwa hamu. Mombasa United inalenga kuanza vyema katika mchujo huo wa mechi mbili ambao unaweza kuamua hatima yao ya kuingia Ligi Kuu; mechi ya kwanza imepangwa kufanyika katika uwanja wa Mbaraki jijini Mombasa na ya pili baadaye jijini Nairobi. Mechi ya marudiano itafanyika Nairobi Jumanne ijayo, huku mshindi kwa jumla ya mabao akipata nafasi katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL).

Jua linashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.