Waziri wa Mambo ya kigeni Musalia Mudavadi amesisitiza tena dhamira ya Kenya ya kuimarisha zaidi ushirikiano wake wa kimkakati na wa kibiashara na Uchina. Akizungumza jana usiku wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Taifa ya China ya mwaka wa 77 jijini Nairobi, Mudavadi alibaini kuwa Kenya pia ina nia ya kupanua ushirikiano na Uchina katika sekta muhimu zikiwemo miundombinu, afya, kilimo, teknolojia na nishati.
MUSALIA MUDAVADI - CELEBRATE