Polisi wamewatia nguvuni watu 25 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa genge la uhalifu linalohusishwa na msururu wa mashambulizi dhidi ya wakaazi wa Kitale na maeneo ya jirani. Washukiwa hao walikamatwa na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kitale wakati wa operesheni maalum ya kiusalama iliyoanzishwa kufuatia ripoti za kuongezeka kwa vurugu na vitendo vya uhalifu. Kwa sasa, washukiwa hao ​​wanazuiliwa na polisi huku maafisa wakikamilisha uchunguzi na taratibu nyingine kabla ya kuwafikisha mahakamani.