Bunge la Taifa limetoa wito kwa Seneti kuharakisha mchakato wa miswada miwili inayolenga kuboresha sekta ya huduma za kilimo, pamoja na kusimamia wataalamu na mafundi katika sekta ya mifugo. Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, John Mutunga, anasema kuwa sheria hizo zinazopendekezwa zitaweka mfumo wa kisheria kwa ajili ya huduma za ushauri katika kilimo, kuhimiza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na teknolojia za kisasa, na kuifanya sekta hiyo kuwa ya kitaalamu zaidi.

JOHN MUTUNGA-BILLS