Chama cha Wazazi kimewataka wasimamizi wa shule kuacha kuwalazimisha wazazi kulipa ada ya masomo ya ziada kinyume cha Sheria ya Elimu ya Msingi. Mwenyekiti wa Chama hicho Silas Obuhatsa anasema Sheria ya Elimu ya Msingi ya mwaka 2026 inapaswa kueleza wazi adhabu kwa walimu wakuu wanaowatoza wazazi karo za ziada. Anasema fedha za masomo zinapaswa kukidhi mahitaji ya shule, huku saa za masomo zikidumishwa kuanzia saa 7:30 asubuhi hadi saa 3:30 jioni.

SILAS OBUHATSA - TUITION