Bao la dakika za mwisho la Carlos Espi liliisaidia Real Madrid kuishinda Elche 3-1 jana usiku, na kuisukuma sawa na Barcelona kileleni mwa LaLiga wakiwa na pointi 15. Bao la kujifunga la Matías Dituro dakika ya 25 liliiweka Madrid mbele, kabla ya Kyllian Mbappe kuongeza la pili dakika ya 33. Abiel Osorio na Fer Nino walisawazishia Elche katika kipindi cha pili, kabla ya Espi kufunga bao la ushindi dakika ya 91. Mechi nyingine za La liga ya siku ya sita zilishuhudia Valecia ikiishinda Alaves 1-0 na kuwa ushindi wao wa kwanza msimu huu, huku Rayo Vallecano ikiishinda Espanyol 2-1.

 

James Rodríguez ametangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa baada ya miaka 15 jukwaani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa na Colombia mnamo Oktoba mwaka 2011 katika mechi dhidi ya Bolivia, ambapo alifunga bao la ushindi. Alikuwa na jukumu kubwa katika timu ya Colombia, akishiriki katika Kombe tatu za Dunia mwaka 2014, 2018 na 2026. Alishinda Kiatu cha Dhahabu katika Kombe la Dunia la 2014, akiwa na mabao sita katika mechi tano, na anaondoka uwanjani akiwa na mabao 31 katika mechi 131.




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kericho, Kisii na Kitale.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.