Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amemkosoa Rais William Ruto kwa kushindwa kumlaani Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar kuhusu matamshi yake yenye utata kuhusu wapiga kura waliofariki na uchaguzi wa 2027. Sifuna amesema matamshi hayo yanapaswa kulaaniwa vikali na uongozi wa UDA, akionya kwamba yanahatarisha kudhoofisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi na kusababisha mashaka kuhusu uaminifu wa uchaguzi wa 2027.
EDWIN SIFUNA - CONDEMN