Wito wa kuwataka Wakenya kudumisha umoja kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao unazidi kushika kasi, huku Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru, akiwa kiongozi wa hivi karibuni kusisitiza umuhimu wa mshikamano wa kitaifa. Gavana Waiguru amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kuruhusu tofauti za kisiasa kuwagawanya, akiwahimiza wananchi kukumbatia umoja na kuishi kwa amani licha ya misimamo yao tofauti ya kisiasa.

ANNE WAIGURU – SIASA