Tume ya IEBC imetangaza zoezi la mwezi mmoja la Usajili Endelevu wa Wapiga Kura katika eneo bunge la Ol-Kalou kufuatia uchaguzi mdogo wa hivi karibuni katika eneo hilo. Kulingana na notisi ya gazeti kutoka kwa tume hiyo, zoezi hilo litaanza Septemba tarehe 21 hadi Oktoba 20 mwaka huu. IEBC ilisema raia wa Kenya wenye umri wa miaka 18 na zaidi ambao wana kitambulisho halali cha kitaifa au pasipoti ya Kenya wanaastahiki kupata huduma za usajili.