Wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma (matatu) wametishia kuondoa magari yao barabarani iwapo bei ya mafuta haitapunguzwa zaidi kufikia mwezi ujao. Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Matatu, Albert Karakacha, anasema bei ya mafuta duniani imeshuka hadi takriban dola 68 kwa pipa, jambo ambalo linapaswa kuonekana katika bei ya mafuta nchini. Anataka bei ya mafuta ipunguzwe hadi kati ya shilingi 140 na 160 kwa lita, akisema bei za sasa zinaathiri vibaya biashara ya matatu na Wakenya wa kawaida.
ALBERT KARAKACHA –MATATUS