Wakaazi wanaoishi katika nyumba zenye nyufa, kuta zilizopinda au dalili za kuporomoka wanashauriwa kuzingatia kuhamia katika majengo salama kabla ya mvua za El Niño. Mtaalamu wa mipango miji, Absalom Ochieng, anasema dalili hizo zinaweza kuashiria udhaifu wa jengo, huku akiwataka wale wanaoishi katika maeneo yenye ardhi oevu au yaliyo katika hatari ya kukumbwa na mafuriko kuchukua tahadhari, hasa pale ambapo misingi ya nyumba ni dhaifu.

BSALOM OCHIENG’ – EL- NINO