Mwanaharakati wa mazingira Isaac Kalua anawahimiza Wakenya kwenda zaidi ya kupanda miti na kuhakikisha inatunzwa hadi kukomaa. Akizungumza wakati wa kuongoza maadhimisho ya Siku ya 'kupanda Miti Kulingana na Umri Wako' (Plant Your Age Day), inayoadhimishwa kila tarehe 14 Septemba, Kalua alisema taasisi na watu wengi hukimbilia kupanda miti lakini hushindwa kuipa uangalizi wa kutosha. Alitoa wito wa kuwepo kwa uwajibikaji zaidi katika kutunza miti ili kupata manufaa ya kudumu ya kimazingira.
ISAAC KALUA - REPORTING