Tume ya Maadili EACC imemkamata afisa wa KRA kufuatia madai ya kuomba na kupokea hongo ili kufuta deni la kodi na utoaji wa Cheti cha Utiifu wa Kodi. Kulingana na EACC, afisa huyo wa Kisumu anadaiwa kudai Shilingi 100,000 kutoka kwa kampuni ya ujenzi ili kufuta deni la kodi lililoonekana katika mfumo wa iTax. EACC ilisema kuwa deni hilo la kodi hapo awali lilionyesha kiasi cha Shilingi milioni 4.5 kabla ya kurekebishwa na kuwa Shilingi 142,230.