Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amemtaka Rais William Ruto kuachana na mipango ya kuzindua mpango wa muda mrefu wa ruwaza ya 2060 na badala yake ajikite katika kutekeleza ahadi zilizomsukuma Ikulu mwaka wa 2022. Sifuna alisema utawala wa Kenya Kwanza umepewa mamlaka ya miaka mitano kutekeleza ahadi zake za kampeni lakini umeshindwa kutimiza, akisema kwamba Wakenya hawapaswi kufanyiwa mpango mwingine wa muda mrefu kabla ya serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili leo.

EDWIN SIFUNA - KAZI