Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameishutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kuweka vipaumbele vibaya, akitilia shaka uamuzi wa kutumia mabilioni ya pesa kununua sare mpya za polisi huku maelfu ya wanafunzi wakipambana na karo za shule na ukosefu wa ajira kwa vijana ukiendelea. Akizungumza huko Meru wakati wa kampeni ya Linda Mwananchi, Owino alidai Sh bilioni 2.5 zilitengwa kwa ajili ya sare hizo, akisema fedha hizo zinaweza badala yake kusaidia kuunda ajira, viwanda na programu za vijana.
BABU OWINO - BADILISHA