Serikali inapanga kuanzisha bonasi za utendakazi kwa wakulima wanaosambaza miwa kwa viwanda vya sukari vya Mumias, Nzoia, Chemelil, Muhoroni, na Sony. Akizungumza mjini Eldoret, Rais William Ruto alibaini kuwa mageuzi yanayoendelea ya kilimo tayari yameongeza mapato ya miwa kutoka shilingi 4,500 hadi 5,500 kwa tani. Alisema kuwa mabadiliko haya ya sera za kimkakati yataongeza pato la wakulima kwa kiasi kikubwa na kuiwezesha Kenya kuwa muuzaji nje wa sukari ndani ya miaka miwili hadi mitatu.

WILLIAM RUTO - BONUS