Mahakama Kuu mjini Murang'a imeipa Shirikisho la Soka la Kenya ruhusa ya kuanza msimu wa Ligi Kuu ya Kenya wa 2026/27. Hata hivyo, ligi hiyo itachezwa chini ya sheria za 2019, badala ya sheria za 2025 zilizotumika msimu uliopita. Uamuzi huo unaweza kuashiria kurejea kwa mchujo wa kupandishwa na kushushwa daraja chini ya kanuni za 2019. Mahakama ilisema kwamba haikuweza kuamua suala la ustahiki katika hatua ya awali, kwani kufanya hivyo kungefanya ombi hilo lisifanikiwe.

 

Wakati huo huo, kesi ya dharau ya mahakama iliyowasilishwa Murang'a dhidi ya Rais wa FKF Hussein Mohammed, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dennis Gicheru na Meneja wa Mashindano Frank Ogolla imefutiliwa mbali.

Vipindi vya anga kavu vinashhudiwa Kisii, Kericho na Kitale.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.