Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ameangazia mafanikio ya mabadiliko ya kidijitali ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi, akibaini kuwa vyeti vya kibali cha polisi ambavyo hapo awali vilichukua miezi kadhaa kutengezwa sasa vinatolewa mara moja au ndani ya siku moja. Akizungumza huko Kiganjo, Murkomen pia alifichua kwamba kituo kijacho cha amri na mawasiliano kitaanzisha kamera za CCTV katika vituo vyote vya polisi kote nchini na kuwezesha kuripoti uhalifu kwa mbali kupitia OB za kidijitali na uchanganuzi wa data wa AI.
KIPCHUMBA MURKOMEN – CAMERAS