Vuguvugu la Linda Mwananchi litazuru Kaunti ya Meru wikendi hii, siku chache baada ya ziara yake katika Kaunti ya Homa Bay kukatizwa na machafuko. Wataongozwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na viongozi wengine huku wakipeleka kampeni yao ya uhamasishaji Meru. Ziara ya Homa Bay ilikumbwa na usumbufu, huku vuguvugu hilo likiwashutumu maafisa wa usalama na viongozi wa kisiasa wa eneo hilo kwa kushindwa kuzuia vurugu wakati wa ziara hiyo.

EDWIN SIFIUNA – MERU