Kaunti ya Kericho imetangaza mipango ya kuajiri wauguzi wapatao 150 kwa muda mfupi huku mgomo wa wauguzi ukiendelea kuvuruga huduma za afya ya umma. Gavana Eric Mutai alisema utawala wa kaunti utatangaza mara moja nafasi hizo za muda kwa nia ya kurejesha huduma katika vituo vya afya vya umma vilivyoathiriwa na mgomo huo. Gavana alisema kaunti hiyo ilikuwa tayari kujaza nafasi ya wauguzi wanaogoma, akisema kwamba wagonjwa hawapaswi kuachwa bila huduma muhimu za matibabu.
ERIC MUTAI – NURSES