Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ameipa huduma ya polisi, TSC na KDF siku saba kufichua maelezo ya ajira zilizofanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kalonzo anataka taasisi hizo zifichue ni watu wangapi waliajiriwa, walikotoka na msingi wa uteuzi wao. Anasema wabunge na mawakili wake watatafuta uingiliaji kati wa mahakama ikiwa mashirika hayo yatashindwa kutoa taarifa hizo. Anasema Wakenya lazima waelezwe ukweli kuhusu ni nani aliyeajiriwa.

KALONZO MUSYOKA – WETANGULA