Viongozi wa kisiasa wanatoa wito wa kukomeshwa kwa uhuni na vurugu zinazofadhiliwa kisiasa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Mwanasiasa wa Mombasa Karisa Nzai na Mbunge wa Eldas Adan Keynan wamewasihi vijana kukataa kutumiwa kusababisha machafuko, wakionya kwamba vurugu za kisiasa zinatishia demokrasia na uchumi wa Kenya. Nzai anasema vijana wanapaswa kuzingatia elimu, ujuzi na ujasiriamali, huku vyombo vya usalama vikilazimika kushughulikia vikali wahalifu.