Mvulana wa miaka minne anauguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi huko Eldoret baada ya kudaiwa kushambuliwa kingono na kudungwa kifuani kwa fimbo kali huko Kasore, Baringo Central. Polisi wamemkamata mvulana wa miaka 16 kuhusiana na tukio hilo na wanatarajiwa kumfikisha mahakamani. Wakaazi wanasema mshukiwa huyo anadaiwa kuhusishwa na tukio kama hilo lililomhusisha mtoto mwingine wiki tatu zilizopita.


VOX POP – BARINGO