Naibu Kamishna wa Kaunti ya Murang’a Mashariki Charles Muriithi amewaonya machifu na viongozi wa jamii dhidi ya kutatua kesi za unajisi wa watoto na ulawiti nje ya mahakama. Muriithi anasema makosa yote ya kingono dhidi ya watoto wadogo lazima yaripotiwe kwa vyombo vya usalama na kushtakiwa kupitia mfumo wa haki. Alionya machifu wanaopatikana wakificha au kuingilia kesi hizo wanaweza kukabiliwa na hatua za kinidhamu.