Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa kuanza ziara ya kaunti tatu kuanzia hii leo. Katika taarifa, Msemaji wa Wiper Ndegwa Njiru alisema ziara hiyo itampeleka Musyoka kupitia kaunti za Kajiado na Taita Taveta kabla ya kuhitimisha na ibada ya kanisa katika Kaunti ya Machakos Jumapili. Kalonzo, ambaye alizungumza kabla ya ziara ya leo, aliitaka IEBC kuhakikisha uwazi na uwajibikaji kuhusu madai yanayozunguka utoaji wa zabuni za mfumo wa usimamizi wa uchaguzi.
KALONZO MUSYOKA – IEBC