Shirika la Amnesty International linatoa wito wa kujitolea upya kwa Katiba ya Kenya, miaka 16 baada ya kutangazwa kwake. Shirika hilo linasema vurugu za kisiasa zimekuwa za kawaida, huku uhuru wa kujieleza na haki ya kuandamana vinakabiliwa na vitisho vinavyoongezeka. Pia linaikosoa serikali kwa kushindwa kutekeleza kikamilifu Sura ya Sita kuhusu uongozi na uadilifu. Amnesty inataka kufuata vikali maamuzi ya mahakama, sheria ya kutekeleza Sura ya Sita na kukomesha ukatili wa polisi. Rais William Ruto kwa upande mwingine anasema hakuna mkenya anayepaswa kupoteza maisha yake kwa kukosoa Serikali.

WILLIAM RUTO – RIGHTS