Baadhi ya wabunge wa ODM kutoka Nyanza wamekataa juhudi za Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua za kupata uungwaji mkono wa kisiasa katika eneo hilo, wakimtuhumu kwa kujifanya mshirika wa jamii hiyo. Wakiongozwa na Mbunge wa Seme James Nyikal, wabunge hao walisema Nyanza haitachukuliwa kama kombe la kisiasa litakalonaswa na madalali wa kikabila kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Walisema eneo hilo litafanya maamuzi kulingana na maslahi yake, uongozi na imani za kidemokrasia.

JAMES NYIKAL - PURSUE