Vijana wanaendelea kubeba mzigo mkubwa zaidi wa maambukizi mapya ya HIV nchini Kenya. Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa Douglas Bosire anasema asilimia 41 ya maambukizi mapya yaliyorekodiwa mwaka wa 2025 yalitokea miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24. Anasema wakati umri unapoongezwa hadi miaka 34, vijana walichangia asilimia 72 ya maambukizi mapya ya HIV, akisisitiza hitaji la hatua zinazolengwa.
DOUGLAS BOSIRE – INFECTIONS