Katibu wa Huduma za matibabu Ouma Oluga anasema Serikali inatekeleza mageuzi ya afya yanayolenga kushughulikia changamoto muhimu zinazowaathiri akina mama na watoto. Anasema kuongezeka kwa mahudhurio katika kliniki za ujauzito ni kipaumbele, huku Serikali ikilenga asilimia 90 ya huduma za ujauzito, ikilinganishwa na kiwango cha sasa cha kitaifa cha takriban asilimia 58. Anawasihi Wakenya kuendelea kujiandikisha katika SHA akibaini kuwa katika Homa Bay pekee zaidi ya elfu 674 wamesajiliwa.
OUMA OLUGA – MOTHERS