Rais William Ruto amewaonya viongozi wa Narok dhidi ya kufadhili ghasia za kisiasa, kufuatia ghasia zilizowaacha watu kadhaa wakiwa na majeraha ya mishale kabla ya ziara yake katika eneo bunge la Emurua Dikirr. Akizungumza wakati wa ziara yake ya maendeleo katika eneo hilo, Rais Ruto alitoa wito kwa uongozi wa kaunti kuzingatia kuunda mazingira ya amani ambayo yangewaruhusu wakaazi kunufaika na miradi ya maendeleo ya kitaifa.

 

WILLIAM RUTO – SPONSOR