Mgomo wa maafisa wa kliniki umeingia siku yake ya 38, huku Muungano wao ukiishutumu Serikali ya Kaunti ya Nakuru kwa kuchelewesha kutiwa saini kwa makubaliano ya kurudi kazini. Mwenyekiti wao wa Kitaifa Peterson Wachira ameonya kwamba muungano huo unaweza kuwaondoa zaidi ya maafisa 50 wa kliniki ambao bado wanatoa huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na upasuaji na mwitikio wa dharura. Wachira anasema hatua hiyo inaweza kuvuruga zaidi huduma za afya ikiwa mzozo huo hautatatuliwa.
PETERSON WACHIRA – COUNTY