Huku Kenya ikiadhimisha miaka 16 tangu kupata Katiba ya 2010, Jaji Mkuu wa zamani David Maraga ametoa wito kwa viongozi wa serikali na upinzani kuitetea, kuitii na kuishi kulingana nayo. Kupitia taarifa kwenye akaunti yake ya X, Maraga aliwakumbusha viongozi kwamba Katiba ilipatikana kwa shida na watu, sio kupitishwa na wenye nguvu, akiwahimiza kila mtu kuheshimu, kulinda na kufuata sheria zake.