Homa Bay na kaunti zingine katika Kanda ya Ziwa zimepongezwa kwa kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya HIV hadi takriban asilimia 15. Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa, Douglas Bosire, anahusisha maendeleo hayo na juhudi za pamoja za serikali za kaunti, wafanyakazi wa afya, jamii na wadau wengine. Bosire anasema mafanikio hayo yanaonyesha umuhimu wa hatua zilizoratibiwa katika kukabiliana na HIV na magonjwa mengine ya virusi, huku akizihimiza kaunti kudumisha kasi hiyo.
DOUGLAS BOSIRE – HOMA BAY