Rais William Ruto ametangaza kuwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Narok unatarajiwa kukamilika katika miezi miwili ijayo. Rais alisema uwanja huo wa ndege utaimarisha muunganisho wa anga hadi Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara, mbuga maarufu ya wanyamapori duniani katika Kaunti ya Narok, na kuongeza idadi ya watalii nchini. Alisema kituo hicho cha Sh milioni 677 kitahudumia abiria wa ndani na wa kimataifa na kusaidia safari za ndege zilizopangwa kila wiki kutoka Masai Mara kupitia Uwanja wa Ndege wa Wilson jijini Nairobi.

WILLIAM RUTO – NAROK