Kenya inaongeza juhudi za kuhakikisha inaondolewa kwenye grey list ya Jopokazi la Kifedha, huku mashirika ya juu ya utekelezaji wa sheria na uhalifu wa kifedha yakipitia mageuzi yaliyoboreshwa. DPP Renson Ingonga aliongoza mkutano wa mashirika muhimu ili kutathmini maendeleo ya Kenya kabla ya hatua inayofuata ya mchakato wa Jopokazi hilo. Mashirika hayo yalipitia maeneo yanayohitaji hatua zaidi, yakiahidi kuimarisha uchunguzi, mashtaka, urejeshaji wa mali na ujasusi wa kifedha ili kupambana na mtiririko haramu wa fedha na ufadhili wa ugaidi.