Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewaonya wanasiasa dhidi ya vitisho, na maneno ya uchochezi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, akisema vitendo kama hivyo vinaweza kusababisha vurugu. Murkomen alisema ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08 zinapaswa kubaki fundisho kwa Wakenya huku nchi ikijiandaa kwa uchaguzi mwingine wenye ushindani mkubwa. Alionya dhidi ya maneno ya kisiasa yanayowalenga wafuasi na mawakala wa vyama pinzani, akisema Wakenya wanapaswa kuwa huru kuwaunga mkono wagombea wao wanaowapendelea bila woga.

KIPCHUMBA MURKOMEN – POLITICIANS