Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ameonya kwamba vurugu za kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2027 zinaweza kuwa na athari kubwa za kiuchumi. Waziri Mudavadi anasema amani huwapa familia, biashara na wawekezaji ujasiri wa kupanga, kuwekeza na kuunda ajira. Alikumbuka vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, wakati maisha yalipotea, familia zilihama makaazi, biashara ziliharibiwa na shughuli za kiuchumi zilivurugika. Mudavadi anasema kuzuia vurugu za kisiasa kwa hivyo si kuhusu kulinda uchaguzi tu, bali pia riziki, uchumi na maisha ya Wakenya.

MUSALIA MUDAVADI – ELECTIONS