Maafisa wapya wa polisi wamehimizwa kubaki bila kuegemea upande wowote kisiasa na kuilinda Katiba huku Kenya ikielekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja akizungumza katika Chuo cha kitaifa cha Mafunzo ya Polisi huko Kiganjo, Kaunti ya Nyeri jana, alisema maafisa wanaojiunga na Huduma ya Kitaifa ya Polisi lazima wawatumikie Wakenya wote bila upendeleo, bila kujali uhusiano wao wa kisiasa, kabila au maslahi yao binafsi.