Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru anasema kaunti hiyo imewekeza Sh milioni 200 katika miradi ya maji inapolenga kupanua upatikanaji wa maji safi na ya bei nafuu. Gavana Waiguru alizungumza huku ujumbe wa Benki ya Dunia na sekta ya maji ya Msumbiji ukitembelea kaunti hiyo ili kupima mfumo wake wa kielektroniki. Ujumbe huo ulitembelea mradi wa Gathigiriri huko Mwea, ambao unachanganya ushiriki wa jamii, ushuru wa bei nafuu, uhifadhi wa maji na teknolojia. Waiguru anasema miradi 38 ya maji inatekelezwa mwaka huu wa fedha, huku zaidi ya 70 ikifanywa kote katika kaunti hiyo.
FAITH WAMBUI – MAJI