Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja anasema mpango wa lishe shuleni wa Dishi na County unatarajiwa kutoa mlo wake wa milioni 100 mwezi Novemba mwaka huu. Mpango huo hadi sasa umetoa milo milioni 85 kwa zaidi ya watoto elfu 324 katika maeneo bunge yote 17. Sakaja anasema kaunti inapanga kupanua mpango huo hadi shule za upili za umma, kwa kutumia jiko zao 17 kuu zilizopo. Anasema mpango huo unalenga kuhakikisha njaa haizuii kujifunza.