Shirikisho la Soka Kenya limelaani vurugu na machafuko yaliyoathiri pambano la FKF Super Cup kati ya Gor Mahia na Tusker FC katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, huku mashabiki na waandishi wa habari wakiripotiwa kushambuliwa wakati wa machafuko yaliyofuatia mechi hiyo. Shirikisho hilo limetoa taarifa hiyo baada ya Tusker kuishinda Gor Mahia 3-1 katika mechi iliyoghubikwa na matukio ya mashabiki kuvamia uwanja, kuharibu mali na kuvuruga kutolewa kwa kombe. Maafisa wa usalama waliwatoa mashabiki kwa gesi ya kutoa machozi na kuwajeruhi wachache huku waandishi wa habari pia wakinyanyaswa na kushambuliwa.
Mwenyekiti wa tawi la FKF la Nairobi West, Rama Omondi, anasema wako tayari kwa msimu mpya na anatumai utakuwa mkubwa na bora zaidi. Rama ambaye aliongoza sherehe ya tawi la Nairobi West aliwashukuru washiriki wote katika kategoria tofauti na kuwatia moyo wengine kufanya kazi kwa bidii zaidi. Baltimore FC ilishinda timu bora ya wanaume huku Thunder Cats ikinyakua tuzo ya wanawake. Martha Mumbua alitunukiwa kocha bora wa wanawake huku Grace Wangui akiwa MVP. Samuel Opiyo wa Baltimore alinyakua kocha bora wa wanaume.
RAMA OMONDI - WEST
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kericho, Kisii na Kitale.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.