Serikali imeipigia upatu timu ya taifa ya Voliboli ya Wanawake kutetea ubingwa wa Afrika wa 2026. Sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo ya ubingwa wa bara zitafanyika katika Uwanja wa Ndani wa Kasarani saa kumi na moja jioni ya leo. Mabingwa Kenya watapambana na Mali na Zambia katika kundi A, huku Misri, Uganda, Burkina Fasso na Senegal wakicheza katika kundi B. Cameroon, Nigeria. Tunisia na Ghana zitapambana katika kundi C, huku Rwanda, Algeria, Congo na Burundi zikipambana katika kundi D. Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera jana Waziri wa Michezo Salim Mvuria alisema haya.
Jua linashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.