Serikali imewaonya wahalifu, wachochezi na wanasiasa wanaochochea mapigano ya mara kwa mara kwenye mpaka wa Kisii-Narok na Transmara kwamba watakabiliwa na hatua za kisheria.  Kamishna wa Kaunti ya Narok Kipkech Lotiatia na mwenzake wa Kisii James Kamau waliahidi kuimarisha usalama wa mashinani na kuwaamuru maafisa kuwakamata wahalifu. Onyo hilo linafuatia mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili, kadhaa kujeruhiwa, mashamba kuchomwa moto na biashara kuvunjika kwenye mpaka wa Kisii-Transmara.

KIPKECH KAMAU - USALAMA