Serikali imeapa kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wa kisiasa, watu binafsi na makundi yanayolaumiwa kwa kuendeleza vurugu miongoni mwa jamii zinazoishi kwenye mpaka wa Kisii-Narok. Kamishna wa Kaunti ya Narok Kipkech Lotiatia na mwenzake wa Kisii, James Kamau walisema serikali haitawavumilia watu binafsi au makundi ambayo vitendo vyao vinatishia amani na kudhoofisha maendeleo katika eneo hilo. Walizungumza jana wakati wa mkutano wa dharura wa usalama huko Nyabitunwa, kufuatia tukio ambalo watu wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mapigano mapya kuzuka katika mpaka wa Kisii-Transmara, Jumapili.
VOX POP – USALAMA