Tume ya NCIC leo inatarajiwa kuzindua Mpango wa Uchaguzi Mkuu wa 2027 Usio na Vurugu, unaoitwa "Uchaguzi Bila Noma." Kampeni hiyo inalenga kukuza uchaguzi mkuu wa amani, usio na vurugu, kuratibu ufuatiliaji wa matamshi ya chuki, na kushirikisha jamii ikiwa ni pamoja na vikundi vya vijana na viongozi wa mashinani ili kulinda mshikamano wa kijamii kote Kenya. Mwenyekiti wa NCIC Askofu Kepha Omae akizungumza kabla ya uzinduzi huo aliwaomba Wakenya kusalia na amani.
KEPHA OMAE – PEACE