Maafisa wa KWS wanawafuatilia watu wanaoaminika kuhusika katika mauaji ya twiga katika Msitu wa Warabo, Kaunti Ndogo ya Wajir Kusini. Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Leheley Jumapili. Kulingana na polisi, maafisa wa KWS walipokea taarifa kutoka kwa umma yapata saa tisa adhuhuri kwamba watu wawili wanaoaminika kuhusika walikuwa wakisafiri kuelekea Msitu wa Warabo. Walipofika eneo hilo, maafisa waligundua kuwa twiga alikuwa ameuawa na nyama yake ikachukuliwa, na kuacha kichwa na mifupa ya mnyama huyo.