Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua amewasihi wanachama wa chama, wagombea na wafuasi kuepuka vurugu na machafuko wakati wa mikusanyiko ya umma, kampeni na kura za mchujo za chama. Akizungumza na vijana nyumbani kwake Wamunyoro, Gachagua alisema ushindani wa kisiasa unapaswa kutegemea mawazo na sera badala ya vitisho au mapambano ya kimwili. Aliwahakikishia wagombea kwamba chama kitafanya uteuzi huru, wa haki na wa kuaminika.
RIGATHI GACHAGUA - ORDERLY